Ikiwa ungependelea kufanya malipo ya mara moja ya Showmax, badala ya kujisajili, unaweza kufanya hivi unapojisajili au kulipia upya usajili wako.
Wateja Wapya
- Tembelea Showmax.com.
- Chagua Jisajili au Anza.
- Chagua mpango wako.
- Telezesha chini hadi sehemu ya Je, unapendelea kufanya malipo ya mara moja?
- Bofya Ona machaguo zaidi ya malipo.
- Chagua Malipo ya Mara Moja.
- Chagua muda ambao ungependa kulipia.
- Weka maelezo yako na Ufungue Akaunti yako.
- Anza kutazama.
Wateja Waliopo
- Nenda kwenye Showmax.com na uingie.
- Nenda kwenye Akaunti kupitia upau wa menyu wa juu kulia.
- Chagua Mipango na Malipo.
- Chagua mpango wako mpya.
- Telezesha chini hadi sehemu ya Je, unapendelea kufanya malipo ya mara moja?
- Bofya Ona machaguo zaidi ya malipo.
- Chagua Malipo ya Mara Moja.
- Chagua muda ambao ungependa kulipia.
- Weka njia zako za kulipa.
- Endelea kutazama.